
Prince Dube
“Uongozi wa Yanga SC umekubaliana mechi ya Jumammosi ambayo itakuwa mechi ya maamuzi itakuwa ni bure isipokuwa jukwaa la VIP A na jukwaa la VIP B haya yatakuwa maalum kwaajili ya wageni waalikwa” Ally Kamwe Meneja wa Habari na mawasiliano Yanga SC
Katika mchezo wa awali Yanga walipoteza kwa kichapo cha Go;o moja kwa sifuri dhidi ya mabingwa wa nchini Silver Strikers matokeo yaliyokuwa tiketi kwa aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Romain Folz
Yanga wanahitaji kuchinda mchezo wa marudiano utakaopigwa Oct 25 Siku ya Jumamosi katika dimba la Benjamin Wiliam Mkapa ili kupata tiketi ya Kufuzu hatua ya makundi katika kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Afrika