
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo.
Akizungumza leo Disemba 16, 2019 na EATV&EA Radio Digital, Chongolo amesema kuwa yeye ameshindwa kuingilia kati mgogoro huo kwakuwa ni jambo ambalo linatakiwa kufuata taratibu za ajira kupitia idara hiyo.
"Masuala yanayohusiana na ajira kuna Taasisi ambazo zimepewa majukumu yakushughulikia ni jambo ambalo linatakiwa kufuata taratibu, mimi nikiingilia hapo nitaharibu mambo, ikitokea kuna mambo yako nje ya mkataba, labda mtu amekatwa NSSF halafu haijapelekwa ama kakatwa kodi na bila kodi hiyo kupelekwea Serikalini hayo tunaweza kuingilia, lakini linapokuja suala la mikataba inabidi kufuatwa kwa utaratibu wa ajira kupitia Idara ya Kazi" amesema DC Chongolo.
Hatua hiyo imekuja baada ya wafanyakazi hao kugoma na kuiomba Serikali iingilie kati ili waweze kupatiwa ufumbuzi katika masuala yao ya malipo, pamoja na mikataba ambayo wanapewa kwa Lugha ya Kiingereza na hawapewi nafasi ya kuisoma na kuielewa.