Thursday , 16th Jan , 2020

MwanaHipHop Stamina, ametaja moja kati ya vitu ambavyo vinafanya ndoa za mastaa kutodumu ni kutopata mpenzi wa kuwavumilia kwa muda mrefu, kutokana na shughuli zao wanazozifanya.

Picha ya mwanaHipHop Stamina

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Stamina amesema ndoa zinakutana na changamoto nyingi, hali inayopelekea kuvunjika kwa sababu hawapati watu waelewa na wavumilivu.

"Ukiniuliza mimi nitakwambia kitu kingine kinachosababisha ni akili zetu zenyewe, unajua shughuli za wasanii ni kutoka hapa na pale, kupata mtu ambaye atakuvumilia kwa muda wote lazima mtu awe ana uelewa na kazi yako unayoifanya, changamoto za wasanii zinajulikana leo unaweza ukawa Mwanza, kesho Dodoma kwa hiyo lazima upate mtu atakayekuelewa" Ameeleza Stamina.

Aidha msanii huyo wa HipHop ameongeza kwa kusema "Inatakiwa kuwe na viwango vya kuelewa na kuheshimu kazi ya mwenziye, kama haitakuwa hivyo utasikia mara leo katembea na huyu, kesho amechepuka na mwingine, mambo ni mengi na ndoa ina vitu vingi na kwa namna moja au nyingine nimepata nafasi ya kujifunza" ameongeza.

Stamina anatamba na wimbo wake wa asiwaze, ambapo amezungumzia mambo ambayo yamemkuta kwenye ndoa hadi kupelekea kuvunjika kwa ndoa hiyo, iliyodumu kwa muda wa mwaka mmoja.