
Laini za simu
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba, imeeleza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka kujiridhisha kama waliosajili laini zao za simu wametumia vitambulisho sahihi.
Na kwamba TCRA wataendelea kutoa onyo kali kwa wale watakaotumia vitambulisho visivyowahusu wakati wa usajili wa laini zao.
Aidha kwa wale waliositishiwa huduma za laini zao, wanaweza kuendelea na utaratibu wa usajili kwa lengo la kurudisha laini zao zilizofungwa au kupata laini mpya.