Wednesday , 5th Feb , 2020

Bosslady wa BongoFleva Lulu Diva, amesema huwa anamtambua mwanaume aliyekuwa naye kwenye mahusiano kama sio mtu sahihi kwake, pale ambapo atashindwa kumpa pesa za matumizi.

Msanii Lulu Diva

Kupitia EATV & EA Radio Digital, Lulu Diva ameweka wazi hilo kwa kusema hawezi kuwa na mwanaume ambaye hampi pesa au hamsaidii kwenye maisha na kumuhudumia.

"Hata ndani ya siku mbili tu nitamtambua kama sio sahihi, endapo atakuwa hanipi pesa, nitajua kwamba huyu sio mtu sahihi kwangu, lazima mwanaume aje na pesa nitakuwa naye vipi kama hana au hanisapoti kwenye maisha na kunihudumia kama mtoto wa kike, kama ana mapenzi ya kweli halafu pesa hana abaki nayo mwenyewe hayo mapenzi " amesema Lulu Diva.

Lulu Diva ameendelea kusema "Lakini pia nikikuona muongo, sio muamifu, nikiona akili zako  hazijakomaa hatuwezi kuwa pamoja,  bora hata awe anamtambua Mungu, busara,hekima kitakuwa kitu kizuri sana, bora ninyimwe vitu vyote ila nisinyimwe hekima" ameongeza.

Kwa sasa Lulu Diva yupo karibu sana na msanii TID, hali ambayo inashangaza wengi kuhisi kama wapo kwenye mahusiano.