Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe.
Mbowe ameuliza swali hilo leo Februari 6, 2020, bungeni Dodoma, katika Mkutano wa 18 wa Bunge la 11, Kikao cha Nane, na kujibiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
"Vyama vya siasa havijazuiliwa kufanya shughuli zake ila tumeweka taratibu muhimu kwa wale viongozi waliopata ridhaa kwenye maeneo yao, ratiba za uchaguzi zitatolewa na kueleza lini shughuli za kampeni zitaanza" amesema Waziri Mkuu.
Aidha Mbowe alihoji ni lini Serikali itaunda tume huru ya Uchaguzi, ambayo itafanya sasa uchaguzi wa mwaka huu kuwa huru na halali, ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alijibu kuwa.
"Tume hii imeundwa kwa mujibu wa sheria, na chombo hichi hakipaswai kuingiliwa na chombo chochote awe Rais wa Nchi, au chama chochote, chombo hiki kipo huru" amejibu Waziri Mkuu.







