
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Kufuatia taarifa yake aliyoitoa leo kwa umma, Waziri Ummy ameeleza kuwa kupona kwa wagonjwa hao watatu kunalifanya Taifa la Tanzania kubaki na wagonjwa 16, ambao wako Arusha, Zanzibar na Dar es Salaam, ambao wote kwa pamoja wanaendelea na matibabu na hali zao ni nzuri.
"Taarifa ya vipimo kutoka Maabara Kuu ya Taifa zinaonesha, mgonjwa pekee wa Arusha kwa sasa hana maambukizi ikiwa ni siku tisa tangu aanze matibabu, bado anaendelea kuwa chini ya uangalizi hadi atakapochukuliwa vipimo vingine siku ya 14 ya matibabu yake, na kuthibitika hana ndipo atakapotangazwa kama amepona" imeeleza taarifa ya Waziri Ummy.