Friday , 22nd May , 2020

Staa wa filamu nchini Elizabeth Michael "Lulu", ameketi kwenye kipindi cha SalamaNa ya East Africa TV, ambapo amefunguka mambo mengi ikiwemo maisha yake, mahusiano, kazi na ile ishu iliyompeleka gerezani.

Staa wa filamu Elizabeth Michael "Lulu"

 

Kuhusu mahusiano yake Lulu amejibu  tuhuma za kuiba mwanaume aliyekuwa naye kwa sasa kutoka kwa mwanamke mwenziye ambapo amesema  "Mchumba wangu nimemfahamu miaka mingi kidogo wakati napenda sana club na yeye alikuwa Dj katika hiyo club, tulikuwa tuna urafiki, tunajuana na hata kwenye mahusiano kuanza haikuwa ngumu, japo nilimkuta ametoka kuwa kwenye mahusiano na nilihakikishiwa kwamba yameisha".

"Sasa hivi tupo kwenye miaka mitano au sita tangu tulivyoanza mahusiano, sidhani kama kutakuwa na kitu kibaya, kama ningemuiba basi ingepita mwaka mmoja halafu angerudi kwa mpenzi wake" ameongeza.

Usiache kutazama kipindi cha SalamaNa, kila siku ya Alhamisi kuanzia saa 3:00 usiku na marudio ni Ijumaa saa 8:00 mchana.