Saturday , 13th Jun , 2020

Ligi kuu ya soka Tanzania bara leo Juni 13, 2020, inarejea kwa mara ya kwanza baada ya kusimama kwa miezi takribani mitatu kutokana na janga la Corona.

Leo inatarajiwa kufanyika michezo miwili ambapo wa kwanza ni kati ya Mwadui FC dhidi ya Yanga SC utakaopigwa uwanja wa Kambarage Shinyanga, huku mwingine ukiwa ni kati ya Coastal Union dhidi ya Namungo FC.

MWADUI FC VS YANGA 

Kuelekea mchezo huu, Yanga wanaingia uwanjani wakiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam FC. Yanga wamecheza mechi 27 na wanapointi 51 huku tofauti ya magoli yao ya kufunga na kufungwa ikiwa ni 11.
Mwadui wao wapo nafasi ya 12, wakiwa wamecheza mechi 28 na kujikusanyia pointi 34, huku wakiwa na deni la magoli matano kwenye tofauti ya kufunga na kufungwa.

Mwadui FC

COASTAL UNION NA NAMUNGO FC

Huu ni mchezo mwingine ambao ni wa kuvutia kutokana na ubora wa hizi timu.
Wenyeji Coastal Union wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi 46 kwenye mechi 28. Tofauti yao ya magoli ya kufunga na kufungwa ni 8.

Coastal Union

Namungo FC wapo katika nafasi ya 4 wakiwa na pointi 50 kwenye mechi 28. Tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni 9.

Namungo FC

Mechi zote zinatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni.