Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara
Waitara ametoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kusema kuwa tangu alipoamua kubadili upepo wa chama cha siasa, alipanga pia kubadilisha jimbo na hivyo msimamo wake uko palepale na Julai 14, ataenda kuchukua fomu ya Ubunge kupitia CCM kwenye jimbo la Tarime Vijijini
"Dar es Salaam sina ninayemkimbia jimbo langu la Ukonga liko salama kuanzia ndani na nje ya chama, nimeshafanya kazi ya kuwasambaratisha CHADEMA hawapo kabisa walikuwa na Meya wa Jiji hayupo, Meya wa Ilala hayupo, mimi nimeshamaliza kazi Dar es Salaam naamini nimefyeka kwenye Sebule, nadhani chumbani ndiyo kuna tatizo hivyo nitafanya siasa mkoani Mara kwenye Jimbo la Tarime Vijijini" amesema Naibu Waziri Waitara.