
Mtia nia wa Ubunge, Jimbo la Kawe na Mhungaji wa Kanisa la Ufufu na Uzima, Josephat Gwajima.
Hivi karibuni Gwajima alisema ametia nia kuomba ridhaa ya chama kugombea na kusema akipata nafasi hiyo atalikomboa Jimbo la Kawe ambalo limekuwa chini ya upinzani kwa muongo mmoja, huku akisema wananchi wa Kawe wamekosa mambo mengi ya manufaa kwenye jimbo hilo ambalo lina watu wengi wasomi, wafanya biashara na wananchi wa kawaida kwa sababu ya kukosa mtu wa kuwaunganisha, jambo ambalo limeleta ugumu katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.
“Nikweli nimetia nia kupitia chama changu CCM na nimejipanga vizuri sijakurupuka na uwezo ninao wakuiongoza Kawe. Chama kikinipa ridhaa” alisema Gwajima.
Gwajima ambaye aliwahi kunukuliwa kukataa kugombea nafasi yoyote ya uongozi kisiasa, adhma yake ya kutaka kugombea Ubunge Jimbo la Kawe ulizua mizozo mtandaoni.