
Bendera za CHADEMA
Majina yaliyotajwa hii leo Agosti 9, 2020, yamehusisha Majimbo 163 kutoka katika kanda 8, ambazo ni kanda ya Kati, Kanda ya Nyasa, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Serengeti, Kanda ya Viktoria, Kanda ya Kusini, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Pwani.
Majina mengine yaliyochaguliwa kuwania ni pamoja na John Heche, wa jimbo la Tarime Vijijini, Ester Matiko Jimbo la Tarime Mjini, Ester Bulaya jimbo la Bunda Mjini, Godbless Lema jimbo la Arusha Mjini, Rebecca Mgondo Arumeru Mashariki, Jimbo la Siha ni Elvis Mos, Moshi Vijijini Lucy Ndesamburo, Rombo ni Patrick Assenga.
Aidha chama hicho pia kimewateua Leonard Ngonyani kugombea jimbo la Namtumbo, Ndanda ni Cator Joseph Mmuni, Nyamagana ni John Pambalu, Upendo Peneza Jimbo la Geita Mjini, Mbeya ni Joseph Mbilinyi, Serengeti ni Catherine Ruge.