
Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, Elias Mwanjala (Pichani) Katika Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini zilizopo Karume Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari wa michezo Makao makuu ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Mwanjala alisema kesi hiyo inaendelea na kufika katika hatua nzuri na kutokana na kukosekana na nyaraka hizo wanalazimika kukutana leo.
Alisema baada ya kukutana na pande zote mbili na kuahidi kuleta nyaraka hizo usiku wa jana na leo Saa 4:30 asubuhi, Kamati hiyo itakutana tena na mchana huenda wakatoa tamko.
"Kesi hiyo inaendelea vizuri, hadi sasa hakuna mshindi pande zote ni 50/50, baada ya kupata nyaraka hizo na tutapokutana tunamaliza kesi hiyo," alisema Mwanjala.
KUWASILI
Saa 7:16 mchana aliingia Mwenyekiti wa Kamari ya usajili Simba huku Saa 7:30 aliwasili Bernard Morrison.
ULINZI
Ulinzi upo mkali huku Polisi wakitanda kila kona na kulikuwa na magari mawili ya polisi moja lilikuwa nje kwa mashabiki na lingine lilikuwa ndani kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.
MAMIA YA MASHABIKI
Mamia ya mashabiki walijitokeza kwa wingi ili kushuhudia hukumu ya mchezaji huyo Morrison.
Mashabiki hao wengine wamevalia jezi nyekundu kwa maana ya Simba na wengine jezi za njano za Yanga.