
Msanii Mbeya Boy Chuma
Sasa kwa taarifa yako wakati anafanya michano hiyo ilirekodiwa na kuwekwa kwenye mtandao wa Youtube ya East Africa Radio, hadi sasa video hiyo imefikisha watazamaji Milioni 1 na kumfanya awe msanii wa kwanza kutazamwa na watu wengi zaidi kati ya wasanii wote waliokuja kwenye dakika 10 za maangamizi.
Kwa kufanikisha hilo team ya East Africa Radio imemfanyia Surprise ya kumpatia keki baada ya kufikisha watazamaji hao na yeye mwenyewe amesema anaishukuru sana Planet Bongo pamoja na team nzima ya East Africa Radio.