Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni.
Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 14, 2020, na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Salum Hamduni, wakati akizungumzia tukio hilo, ambapo mpaka sasa hivi hakuna mtu yeyote ambaye amekamatwa kuhusika na tukio hilo.
"Mpaka sasa hivi hakuna mtu yeyote ambaye amekamatwa kuhusianaka na tukio hilo na sisi Jeshi la Polisi tunaendelea na uchunguzi ili kuweza kuwabaini wote waliohusika ili hatua za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa, nitoe wito kwa wananchi kutoa ushirikiano na kutupatia taarifa sahihi ili tuweze kuwakamata wahusika", amesema Kamanda Hamduni.
Ofisi za CHADEMA Kanda ya Kaskazini, zimechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo, ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene, hata mlinzi wa ofisi hiyo naye hajulikani alipo.




