
Kushoto ni Pep Guardiola, katikati ni wachezaji wa Lyon na kulia ni Lionel Messi
Baada ya ushindi huo wa Lyon rasmi sasa rekodi ikawekwa kwa vilabu vya England na Hispania kutokuwepo kwenye nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1995-96.
Jumla ya timu nne kutoka mataifa ya Ujerumani na Ufaransa (PSG, Lyon) (RB Leipzig, Bayern Munich) zimebaki kwenye nusu fainali ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu wa 2012-13 ambapo nusu fainali ilihusisha timu kutoka mataifa mawili tu ambayo ilikuwa ni Hispania (Barcelona na Real Madrid), Ujerumani (Bayern na Dortmund.
Rekodi nyingine ni kwa kocha wa Man City Pep Guardiola kupoteza mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa tangu alipojiunga Man City katika misimu ya 17-18, 18-19 na 19-20. Hii ni rekodi mbaya zaidi tangu awe kocha kwani akiwa na Barcelona na Bayern katika misimu yake 7 alivuka hatua hiyo.
Maxwel Cornet sasa ameungana na Lionel Messi kuwa wachezaji walioifunga Man City magoli mengi ikiwa chini ya Pep Guardiola ambapo kila mmoja amefunga magoli manne.