Monday , 31st Aug , 2020

Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete amevitaka Vilabu vya Simba na Yanga kuwekeza katika soka la Vijana ili kuendeleza soka la Nchi.

Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete (Pichani).

Rais Kikwete aliyesema hayo wakati wa kilele cha Tamasha ya wiki ya Mwananchi lililohitimishwa jana katika Uwanja wa Mkapa kwa shughuli mbalimbali za burudani ambalo lilitangulizwa na utambulisho wa wachezaji wapya waliosajiliwa na kikosi cha Yanga.

Akizungumza muda mchache kabla ya mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Eagle Noir ya Burundi ambayo ilimalizika kwa ushindi kwa wanajangwani kwa bao mbili kwa sifuri,Rais Kikwete alisema msingi wa soka bora unajengwa kwa kuwawezesha vijana.

Vilevile aliongeza kuwa masuala ya kuibiana wachezaji hayajaanza leo,kwa kuwa miaka ya zamani Yanga na Simba walikua na tabia hizo,hivyo akawataka Yanga kama waliibiwa Morrison na wao wakaibe mwingine.

Hivyo suala la Benard Morrison lisiwasumbue bali wajipange na wao wakaibe mwingine kwa upande wa Simba na hayo ndio maisha ya Simba na Yanga.