Thursday , 17th Sep , 2020

Rais wa Marekani Donald Trump(Kulia) na Gianni Infantino (Kushoto) walipokutana Ikulu ya USA.

Rais wa FIFA, Gianni Infanino(Kushoto) na wa Marekani Donald Trump (Kulia) kwa pamoja wakiwa Ikulu (White House)

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino mapema leo amekutana na Rais wa Marekani Donald Trump kujadili juu ya mustakabali wa michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2026 inayotarajiwa kufanyika nchini Marekani pamoja na nchi jirani za Mexico pamoja na Canada.

Tenda ya nchi hizo ya kuandaa fainali hizo za kombe la dunia ilipitishwa na wajumbe wa Shirikisho la soka dunia FIFA mwaka 2018 kwa kupata ushindi kwa kupigiwa kura 134 na kuwapiku wapinzani wake Morocco waliopata kura 65.

Infantino na Rais Trump pia wameongea kuhusu kuanzisha makao makuu ya shirikisho hilo la soka duniani FIFA nchini marekani vile vile walifanya mapitio ya ukamilifu wa maandalizi ya mashindano hayo makubwa soka duniani.

Ikukmbukwe kwa mara ya mwisho Marekani ilikua mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 1994.

Infantino pia alitembelea ofisi za utoaji haki za marekani “US Deparetment of Justice' na kuyashukuru mashirika ya Nchi hiyo kwa kazi yao nzuri ya kupingana na rushwa katika mpira wa miguu.

Rais wa Fifa, Gianni Infantino amekutana na rais wa Merika Donald Trump kujadili Kombe la Dunia la 2026, ambalo litafanyika kwa pamoja nchini humo pamoja na Mexico na Canada.

"Tangu nilipochaguliwa, tumeonyesha dhamira yetu ya kutokomeza vitendo vibaya ambavyo vilichafua sifa ya Fifa hapo zamani.

"Tumesisitiza nia yetu ya kushirikiana na kusaidia mamlaka katika uchunguzi wao na mashtaka ya rushwa, ambayo haina nafasi katika mpira wa miguu." Infantino pia alihudhuria kusainiwa kwa makubaliano ya kihistoria kati ya Bahrain, Israel na Falme za Kiarabu, ambayo yalifanywa katika Ikulu ya White House.