Sunday , 20th Sep , 2020

Msanii wa zamani wa BongoFleva Fetty Sley amefunguka kuhusu ujio wake mpya, kupotea kwake, tofauti ya muziki wa zamani na wa sasa, pia amemtolea mfano msanii aliyetamba zamani Mr Nice.

Wasanii wa BongoFleva Fetty Slay na Mr Nice

Akifunguka hilo kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa TV, amesema muziki unakwenda na muda ndiyo maana zamani alikuwepo msanii kama Mr Nice ambaye alifanya vizuri na sasa hayupo, pia zamani hawaku-enjoy muziki kabisa kwa sababu waliufanya tofauti.

"Mr Nice ni mfano mzuri wa neno muziki ni muda, alikuwepo na sasa hayupo ila kitu kilichofanya nipotee kwa muda ni maisha nje ya muziki, kuna vitu vingi vya kufanya ndiyo maana baada ya kutulia nimerudi tena, naweza nisiwike sasa hivi ila baadae nikawika" amesema Fetty Sley

Pia ameendelea kusema "Zamani haikuwa rahisi kabisa ku-enjoy muziki kwa sababu tulifanya muziki kama kazi ila sasa ni biashara na bado inakuwa ngumu kutoboa kutokana na muda na mabadiliko katika tasnia".

Zaidi tazama hapa chini.