Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Chadema yaahidi kufufua zao la Pamba Tabora 

Sunday , 20th Sep , 2020

Mgombea mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu amesema iwapo chama hicho kitaingia madarakani kitahakikisha watu wa mkoa wa Tabora wanarudishiwa kilimo cha zao la pamba na kuhakikishiwa upatikanaji wa soko la zao hilo.

Mgombea mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu.

Mgombea mwenza huyo ameyasema hayo leo Septemba 20, 2020, wakati akinadi sera za chama hicho katika mkoa huo ambapo pia amewaahidi watu wa Tabora upatikanaji wa maji safi, elimu bora pamoja na masoko ya mazao ya tumbaku na pamba.

Watu wa Tabora Kaskazini mkituchagua tutahakikisha tunawarudishia zao lenu la pamba na tutahakikisha pamba yenu mtaweza kuuza sehemu kwa yeyote mnayemtaka sio kwenye vyama vya ushirika vinavyowakopa pamba yenu,’’alisema Salum Mwalimu na kuongeza.

“Hiki ni kipindi cha kupanga upatikanaji wa elimu bora, upatikanaji wa maji safi, soko la tumbaku yetu na upatikanaji wa soko la pamba yetu,’’.

Aidha, mgombea huyo mwenza wa Chadema amesema kwa sasa chama hicho ndio chenye Ilani bora ambapo amewaomba wananchi kukichagua chama hicho ili waweze kuleta mageuzi ya kiutawala, kiuchumi na kijamii.

HABARI ZAIDI

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP