Thursday , 12th Nov , 2020

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Novemba 12, 2020, limemthibisha Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania 2020-2025. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akipongezwa na wabunge

Akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa na wabunge, Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Majaliwa amepigiwa kura 350 na hakuna kura iliyoharibika hivyo amepitishwa kwa asimilia 100%.

Mapema leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, alipendekeza jina la Mbunge huyo wa jimbo la Ruangwa Mh. kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika awamu yake ya pili ya uongozi (2020 -2025).

Baadaye Mwanasheria Mkuu wa Serikali Adelardus Kilangi, aliwasilisha hoja mbele ya bunge ya kuthibitisha uteuzi na bunge limefanya hivyo.