Thursday , 12th Nov , 2020

Gwiji wa Argentina, Diego Maradona ameruhusiwa kutoka hospitalini jana na kupelekwa kwenye kliniki ya matibabu ya kuishi bila utegemezi wa pombe.

Diego Maradona (Kushoto) akimpongeza Lionel Messi(kulia) enzi anaifundisha timu ya taifa ya Argentina.

Maradona, ambaye aliongoza nchi yake kushinda Kombe la Dunia mnamo 1986, alifanyiwa upasuaji mzuri wa kuganda kwa damu kwenye ubongo mapema Novemba mwaka huu.

"Jambo zuri ni kwamba Diego yuko pamoja, Diego yu dhabiti," wakili wake, Matias Morla, alisema.

Nyota huyo wa zamani alilazwa katika kliniki ya Ipensa huko Buenos Aires wiki iliyopita kutokana na tatizo la upungufu wa damu na maji mwilini. Ni marafiki wachache tu wa karibu wataruhusiwa kumtembelea nyota huyo mwenye miaka 60 kwenye kliniki mpya aliyolazwa.