
Muigizaji na mshehereshaji MC Zipompa enzi za uhai wake
Ratiba ya mazishi inaeleza kuwa mwili wake utaanza kuagwa kwenye viwanja vya Karimjee kuanzia 2:00 hadi 3:00 asubuhi, kisha itafuata ibada, salam za rambirambi na makala ya maisha yake.
MC Zipompa alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 10 baada ya kuzidiwa na maradhi ya ghafla akiwa nyumbani kwake Mbweni kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Rabininsia iliyopo Tegeta Dar Es Salaam, ili kuokoa maisha yake lakini bahati mbaya ikashindikana.