Saturday , 14th Nov , 2020

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bi,Zipora Liana imesema imefuatilia utekelezaji wa mradi wa stendi mpya ya mabasi mbezi na kufanikiwa kudhibiti zaidi ya shilingi bilioni 12 .

Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU Jenerali John Mbungo

Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za TAKUKURU Mkurugenzi Mkuu Jenerali John Mbungo amesema fedha hizo ambazo zimedhibitiwa  zingeweza kulipwa kwa wakandarasi kama ziada kwa kazi ambayo haijafanyika.

"Uthibiti huu umefanyika kwa kuwa wachunguzi na wataalamu wa ujenzi kutoka TAKUKURU wamekuwa wakifuatilia kazi hii kwa karibu"amesema Jenerali John Mbungo

Aidha Jenerali Mbungo amekabidhi fedha kwa Mkaguzi wa idara ya ukaguzi wa ndani Rehema Mkumbwa  kutoka Shirika moja la kimataifa lisilo la Kiserikali kiasi cha shilingi milioni 118, ambazo zilichepushwa kwa njia ya udanganyifu kutoka katika shirika hilo.

Katika hatua nyingine Takukuru inawashikilia  watumishi wa nne wa mfuko wa taifa wa bima ya afya nhif kwa mahojiano kwa ubadhilifu wa fedha kiasi Cha shillingi za kitanzania million 500.4 ambapo hatua za kisheria zitachkuliwa kwa watakaothibitika.