Tuesday , 17th Nov , 2020

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,  Joseph Mafuru, amesema ongezeko la watu katika jiji hilo limechangia kwa kiasi kikubwa kukua wa shughuli za kiuchumi pamoja na ongezeko la fursa mbalimbali.

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,  Joseph Mafuru

Akizungumza katika kipindi cha Supa Breakfast ,leo, Mafuru amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia na kutekeleza adhma ya jiji la Dodoma kuwa makao makuu.

"Ongezeko la watu limechochea shughuli nyingi za kiuchumi kukua katika jiji la Dodoma na kumekuwa na fursa mbalimbali ambazo hazikuwepo hapo awali, Mheshimiwa Rais John Magufuli, na serikali yake wameweka miundo mbinu ya kutosha katika jiji hili, jiji hili lina uhakikia wa usafiri kuna ndege, treni, mabasi ya abiria" amesema Mafuru

Aidha Mafuru amewaalika wawekezaji kwenye sekta ya kiwanda kufika katika jiji hilo kwa ajili ya uwekezaji kwani kuna ardhi ya kutosha Dodoma.

“Suala la ardhi Dodoma sio shida na ofisi yangu imejidhatiti kuhakikisha inapokea wawekezaji hivyo wawekezaji wanaofikiria kuanza viwanda vidogovidogo, vya kati na viwanda vikubwa, vile viwanda vinavyohitaji zaidi ya ekari 250 zipo na tayari tumezipima" amesema Mafuru