
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa
Majaliwa ameyasema hayo mara baada ya kufanya ukaguzi wa karakana hiyo na kulipongeza shirika la reli Tanzania (TRC) kwa kazi nzuri wanayoifanya mbapo pia amewaahidi watanzania kuwa miradi yote ya kimkakati ikiwemo ya reli Serikali itahakikisha inakamilika.
“Lazima kuwe na hoteli lazima kuwe na nyumba za kulala wageni , kuwe na maeneo ya masoko ya kibiashara , kuwa na maeneo ya usafiri mdogomdogo wa kuunganisha vijijini kuja hapa, taxi, bodada lazima litengwe eneo na mkurugenzi unanisikia hapa ninapo hesabu hesabu hayo ndio mambo muhimu mazingira yote yatengenezwe kila mtu anufaike ” amesema Waziri Majaliwa
Aidha Majaliwa ameweka wazi kuwa ana ridhishwa na kasi ya ujenzi wa karakana ya utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni unaoendelea katika eneo la Kwala mkoani Pwani huku akisema kuwa huo ni mji mpya wa baadaye endapo mambo yote aliyoyasema yatafanyiwa kazi.