Monday , 21st Dec , 2020

Mhadhiri  kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. George Kahangwa  amesema viongozi  wanaohitaji kukumbushwa kuhusu kuwa na mpango kazi wanalikosea taifa.

Mhadhiri  kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. George Kahangwa

Akizungumza katika Kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio Dkt.Kahangwa amesema kuwa kutoikujua kuhusiana na mpango kazi ndio chanzo chakuwa na watendaji wasiojua wana wajibu gani wa kutimiza kwa taifa matokeo yake hawana la kufanya zaidi kukaa maofisini.

“Suala la mpango kazi halipaswi kiongozi akumbushe ni utaratibu wa kawaida wa kila ofisi hawa wanaohitahji kukumbushwa kuwa na mpango kazi kwa kweli wanalikosea taifa na ndio maana watu wakati mwingine hawajuui wafanye nini”  amesema Dkt. Kahangwa

“Mpango kazi ni jambo la kusisitiza sana kwani mambo ya mpango kazi yanaaibisha yakiwa yanazungumziwa katika ngazi za juu ilhali kuna viongozi ambao  wapo wanaotakiwa wawakague wenzao wa chini kuhusiana namipango kazi yao” ameongeza Dkt. Kahangwa  

Aidha Dkt.Kahngwa amesifu tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli  kuhusiana na kufundishwa histori ya kwetu ambapo amesema kufanya hivyo kutasaidia kizazi hadi kizazi  kujua tunapotoka  na jambo tunalolifanya leo msingi wake ni upi kuliko kuwafundisha vitu ambavyo haviwakumbushi uzalendo wala  chimbuko lao.