Wednesday , 23rd Dec , 2020

Ni 'headlines' za msanii wa filamu Duma Actor ambaye ameingia rasmi kwenye muziki baada ya kutoa wimbo wake wa kwanza ambapo amesema kama lebo ya Kings Music ya Alikiba au Konde Gang ya Harmonize wanataka kumsaini kwenye lebo zao basi waandae mzigo wa kutosha.

Msanii wa filamu na muziki Duma Actor

Akizungumza hayo kwenye kipindi cha PlanetBongo Duma Actor amesema kuwa "Huu ni wimbo wangu ya kwanza ila nishafanya kazi ya muziki zamani kabla ya kuingia kwenye filamu, hata wanamuziki nao wanatamani kuingia kwenye uigizaji kama Q Chief na Mr Blue tayari wameshafanya hivyo"

"Ujue mimi ni mchaga naangalia pesa kwanza, kama Alikiba na Kings Music yake au Harmonize na Konde Gang wanataka kunisaini kwenye lebo zao nitaangalia wapi ambapo kuna mzigo zaidi ndiyo nitaenda" amesema Duma Actor 

Duma Actor anafuata nyayo za Hamisa Mobetto ambaye na yeye aliwahi kuwa msanii wa filamu, video vixen kisha kuingia kwenye muziki.