
Kocha mwenye maneno mengi Jose Mourinho
Amesema ''ukame wa mataji kwa Spurs uliodumu miaka 13 tangu walivyotwaa ubingwa wao wa mwisho wa kombe la ligi mwaka 2008 sasa basi, nimewandaa vizuri vijana wangu na tumezungumza umuhimu wa kutwaa kombe hili kwa kuanzia, nashukuru wachezaji wangu wamenielewa sasa ni zamu yetu''.
Totternham watakuwa wanamsubiri mshindi yeyote kati ya Manchester United dhidi ya Manchester City, ambao wanacheza nusu fainal yao leo tarehe 6/1/2021, saa 4:45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Jose Mourinho ni moja ya makocha wenye mafanikio ya juu kisoka, akiwa ametwaa jumla ya makombe 20, katika ngazi ya ligi za ndani na ile ya mabingwa wa Ulaya, akiwa na vilabu tofauti tofauti kwa karibu miongo miwili kuanzia 2000.
Mourinho alichukua nafasi ya Mauricio Pochettino aliyetimuliwa kazi mwezi Novemba 2019, huenda akawa tiba sahihi kwa Spurs yenye kiu ya mafanikio kwa muda mrefu. Fainali ya kombe la Carabao inatarajiwa kuchezwa tarehe 25/4/2021 katika uwanja wa Wembley.