Saturday , 16th Jan , 2021

Uchaguzi wa kumchagua rais mpya wa klabu ya Barcelona uliopangwa ufanyike tarehe 24 mwezi huu umesogezwa mbele na sasa utafanyika tarehe 7 machi 2021 baada ya bodi ya klabu hiyo kusema wamefanya hivyo ili kukepa mikusanyiko kipindi hiki ambacho maambukizi ya Covid-19 yameshamiri.

Carles Tusquets anayokaimu nafasi ya Urais wa klabu ya Barcelona kwa sasa.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya bodi na wagombea wote watatu wa Urais klabuni hapo kuketi na kukubaliana kutovunja sheria kutoka mamlaka za ustawi wa jamii zinazotaka watu nchini Hispania kukwepa mikusanyiko ili kukwepa uwezekano wa kueneza Covid-19.

Baada ya taarifa hiyo kuthibitishwa na Carles Tusquets anayekaimu nafasi ya Rais klabuni Barcelona baada ya Jose Batromeu kujiuzulu miezi mwishoni mwaka jana, Barcelona imesema kuna uwezekano mkubwa sana usajili wa Mlinzi Erick Garcia kutoka Man City ukasubiri hadi uongozi mpya upatikane.

Kwa Upande mwingine, Mchezaji nyota wa klabu hiyo Lionel Messi amezidi kumpasua kichwa kocha wake Reonald Koeman baada ya nyota huyo kushindwa kufanya mazoezi ya jana wakati Barcelona ikiwa inajiandaa kukipiga na Athletic Bilbao kwenye finaili ya Spanish Super Cup kesho jumapili.

Messi anayesumbuliwa na maumivu ya misuli aliukosa mchezo wa mtoano wa Barcelona dhidi ya Real Sociedad ulichozwa jumatano ya wiki hii na Barcelona kufuzu kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-3.