Saturday , 16th Jan , 2021

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda, imemtangaza Yoweri Museveni, kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais wa nchi hiyo baada ya kupata kura 5,851,037, sawa na 58.64%.

Yoweri Museveni, Rais mteule wa Uganda.

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda, imemtangaza Yoweri Kaguta Museveni, kuwa mshindi wa kiti hicho kufuatia uchaguzi uliofanyika Januari 14, 2021, ambapo amemshinda mpinzani wake Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine aliyepata kura 3,475,398 sawa na asilimia 34.83 ya kura zote.

Yoweri Museveni, anachaguliwa kuliongoza Taifa hilo la Uganda kwa zaidi ya miaka 30 sasa, tangu aliposhika nafasi hiyo mwaka 1986.