Monday , 18th Jan , 2021

Lionel Messi usiku wa jana  tarehe 17/1/2021 aliadhibiwa kwa kadi nyekundu, katika mchezo wa fainali ya  Super Cup ya Hispania iliyowakutanisha Barcelona dhidi ya Athletic Bilbao, ikiwa ni kadi yake ya kwanza tangu aanze kuitumikia Barcelona mwaka 2004.

Nahodha wa Barcelona Lionel Messi

Messi ambaye pia ni nahodha wa timu ya Barcelona pamoja na timu ya Taifa ya Argentina, aliadhibiwa kwa kadi nyekundu katika dakika ya mwisho ya mchezo huo wa fainali, uliochezwa kwa dakika 120 na kumalizika kwa Bilbao kuibuka na ushindi wa 3-2 na kutwaa ubingwa.

Hii si mara ya kwanza kwa Lionel Messi mshindi mara 6 wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d'Or), kuadhibiwa kwa kadi nyekundu, kufanya  kuwa na jumla ya kadi nyekundu 3, mbili zikiwa kwenye timu ya taifa Argentina  na moja ndiyo hii kwenye klabu.

Messi ameitumikia Barcelona kwa miaka 17 kwa kucheza jumla ya michezo 753 na kuadhibiwa kadi nyekundu 1 tu, na pia  mwamuzi Gil Manzino ameingia kwenye rekodi ya kuwa Mwamuzi wa kwanza wa uhispania kumpa kadi hiyo nyekundu.