Sunday , 24th Jan , 2021

Mtendaji Mkuu wa klabu ya soka ya Simba SC Barbara Gonzalez, leo Januari 24, 2021, amemtangaza Didier Gomes Da Rosa kuwa Kocha Mkuu mpya.

Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez akimkabadhi jezi ya mabingwa wa nchi Kocha Mkuu mpya Didier Gomes Da Rosa.

Didier Gomes Da Rosa ambaye ni raia wa Ufaransa alikuwa kocha wa klabu ya Al-Merrikh SC na sasa rasmi amechukua mikoba iliyoachwa wazi na Sven Vandebroek kuinoa Simba.

Kwa upande wake Didier Gomes Da Rosa, amesema “Timu niliyoondoka niliamua mwenyewe. Nataka kuwepo Simba kwa muda mrefu. Nina furaha sana kuwa hapa na tuna nafasi ya kufanya mengi pamoja mbeleni.”

Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Kocha Mkuu mpya Didier Gomes Da Rosa wakisaini mkataba mbele ya waandishi wa habari.

Hata hivyo licha ya kusaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari lakini haujawekwa wazi ni wa muda gani.

Chini ni vilabu alivyopita pamoja na muda aliokaa.
2013-2014 Rayon Sports
2014-2015 Coton Sports
2015-216 CS Constantine
2016-2017 JSM Skikda
2017-2018 Ethiopian Coffee
2019- Horoya AC
2019-2020 Ismaily
2020- Al Merrikh