Sunday , 24th Jan , 2021

Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde ameagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini kwa kukosa madawati au kusoma chini ya miti kwa upungufu wa madarasa na kuagiza ujenzi wa madarasa-

Picha ikiwaonesha wanafunzi kutoka moja ya shule nchini (picha na mtandao) kulia ni Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde.

katika wilaya zote uanze mara moja kwa yale maeneo yenye upungufu wa madarasa.

Silinde ametoa maagizo hayo alipotembelea shule ya msingi King'ongo iliyopo wilaya ya Ubungo mkoa wa Dar es Salaam kufatia agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka ujenzi wa madarasa ya shule hiyo ukamilike kwa haraka, baada ya kuona video ya watoto wa shule hiyo wakisoma chini ya mti.

Silinde amesema serikali ilitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa maeneo mengi ya nchi katika mradi wa lipa kwa matokeo EP4R tangu mwezi wa Juni, 2020 lakini madarasa bado hayaja kamilika katika baadhi ya maeneo lakini kwa ujenzi wa madarasa katika shule ya King'ongo utakamilika ndani ya wiki zisizozidi tatu na kutaka watendaji katika wilaya zote kukamilisha ujenzi bila kusukumwa na viongozi wa kubwa wa nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo  Beatrice Dominic amemwambia Naibu Waziri wa TAMISEMI kuwa ujenzi wa madarasa huo utakamilika Januari 31, 2021 na hadi Februari  5, wanafunzi wataanza kuyatumia madarasa hayo na mpaka kukamilika yatatumia zaidi ya shilingi milion 205 yakiwa ni ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa ambavyo vitakuwa na madawati yake pamoja ujenzi wa choo chenye matundu 12.