
Uwanja wa Azam Complex
uwanja huo kwenye michezo ya kombe la shirikisho.
Klabu ya Namungo ambayo ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika awali ilikuwa inatumia uwanja wa Azam Complex kwenye michezo yake ya nyumbani, lakini kwa sasa wamepokea maelekezo kutoka shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kwamba michezo yao yote ya nyumbani ya hatua ya makundi ichezwe katika dimba la Benjamin Mkapa.
Baada ya taarifa hizo kusambaa kuwa huenda uwanja wa Azam Complex ambao ni uwanja wa nyumbani wa Azam FC umekosa vigezo na umefungiwa, Afisa habari wa wamiliki wa uwanja huo Zaka za Kazi ametolea ufafanuzi juu ya taarifa hizo.
“Sisi kama klabu hatujapewa taarifa yoyote, japo tumewasiliana na Namungo ambao wao ndio walikuwa wanatumia uwanja huu na wao wamesema kwamba wamepewa maelekezo kwamba mechi zao za hatua ya makundi za nyumbani wacheze katika uwanja wa Benjamin Mkapa, lakini hawajaambiwa sababu zozote za kuhamisha mechi zao.”
Taarifa hiyo ya Zakaria ikafafanua zaidi kuwa bado hawajapokea taarifa rasmi kutoka CAF.
“Sasa sisi kama klabu ambao wamiliki wa uwanja tunasubiri taarifa rasmi kutoka CAF, na maelekezo ili tuchukue hatua kuufanya uwanja wetu uwe na vigezo vyote vinavyotakiwa, lakini hadi tukio hili linakuja uwanja wetu ulipitishwa na CAF kwa ajiri ya mashindano ya Afrika tangu mwaka 2014.”