
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe
Kauli hiyo inafuatia kuwepo kwa majimbo yaliyoachwa wazi kutokana na wabunge wake mmoja kuteuliwa katika nyadhifa za juu zaidi na mwingine kufarikia dunia.
Kabwe amesema wanachama wake wapo tayari katika kushiriki na watashiriki kikamilifu uchaguzi na kampeni katika majimbo hayo mawili.
Majimbo yaliyoko wazi ni la Buhigwe ambalo mbunge wake alikuwa Dkt. Philip Mpango ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Tanzania na la Muhambwe ambalo mbunge wake alikuwa marehemu Eng. Atashasta Justus Nditiye.
Kauli ya Zitto inakuja mara baada ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukaa kikao tarehe 31/03/2021 na kutoa tamko la kutoshiriki katika uchaguzi mdogo kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu Chadema Benson Kigaila.