
Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar
Mabao ya Simba yamefunga na Clatous Chama dakika ya 9, Rally Bwalya dakika ya 19, Meddie Kagere amefunga mara mbili dakika ya 43 na 52 na Miquissone akaifungia Simba bao la tano dakika ya 69.
Kwa ushindi wa hii leo wekundu wa msimbazi wamepanda kwa nafasi moja kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili na wameishusha Azam FC, sasa kikosi hicho kimefikisha alama 49 ikiwa ni tofauti ya alama mbili tu na vinara wa ligi Yanga wenye alama 51. Mtibwa Sugar wamesalia nafasi ya 15 wakiwa na alama 24.
Na mabao mawili aliyofunga Kagere leo yamemfanya kukwea mpaka kileleni na kuwa kinara kwenye orodha ya wafungaji amefikisha mabao 11, akifuatiwa na Prince Dube wa Azam FC mwenye mabao 10.