Tuesday , 20th Apr , 2021

Nyota wa Golden State Warriors ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika NBA mwenye umri wa miaka 33+ kufunga alama 30 na zaidi katika michezo 11 mfululizo.

Nyota wa Golden State Warriors , Stephen Curry(Kushoto)Pichani akionyesha umahiri wake katika moja ya mchezo wa NBA.

Curry alifunga alama 49 wakati Golden State Warriors ikiifunga Philadelphia 76 ers kwa alama 107-96 usiku wa kuamkia leo.

Hayari, Kobe Bryant alikuwa akishikilia rekodi ya kufunga alama 30 na zaidi katika umri huo alipofanya hivyo katika michezo 10 katika msimu wa 2012.

Nyota huyo alifunga alama 40 mara tano katika ndani ya mwezi April, na kuwapiku Michael Jordan na hayati Kobe Bryant ya kuwa mchezaji mwenye umri wa zaidi ya miaka 33 ambaye amefunga mara ngingi alama 40 ndani ya mwezi .

MATOKEO YA JUMLA
Cleveland Cavaliers 105-109 Dertoit Piston
Chicago Bulls 102-96 Boston Celtics
San Antonio Spurs 109-96 Indiana Pacers
Houston Celtics 91-113 Miami Heat
Oklahoma City Thunder 107-119 Washington Wizard
Phoenix Suns 128-127 Milwaukee Bucks
Memphis Grizzlies 137-139 Denver Nuggents
Utah Jazz 111-97 Los Angeles Lakers

FAHAMU WACHEZAJI WALONG'ARA
Wachezaji waliong'ara zaidi katika michezo ya alfajiri ya leo ni Stephen Curry wa Golden State Warriors aliyefunga alama 49 akifuatiwa na Nikola Jokic wa Denver Nuggents aliyefunga alama 47 wakati timu yake ikiiadhibu Memphis,huku nafasi ya tatu ikuchukuliwa na Giannis Atetokounmpo wa Milwaukee Bucks aliyefunga alama 33 licha ya timu yake kupoteza dhidi ya Phoenix Suns.