
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali itaendelea na utanuzi wa viwanja vya ndege pamoja na kulilea kimkakati Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili liweze kujiendesha kwa ufanisi zaidi.
Akihutubia Bungeni leo Jijini Dodoma, Mhe. Samia amesema kuwa wanakwenda kufanya utafiti ili kuhakikisha wanaoliendesha Shirika la ATCL ni watu wenye uweledi na uwezo wakuliendesha shirika hilo kibiashara.
“Tutaendelea na utanuzi wa viwanja vya ndege na kujenga Uwanja wa Kimataifa wa Msalato hapa Dodoma, aidha tutaendelea kulilea shirika letu la ndege la ATCL kimkakati ili liweze kujiendesha kwa ufanisi,” amesema Rais Mhe. Samia.
Rais Samia ameongeza kuwa serikali haitokubali kuliona shirika hilo linatengeneza hasara kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika shirika hilo "Kama serikali tunakwenda kulitua mzigo mkubwa wa madeni shirika letu la ndege na kulipa unafuu wa kodi na tozo ili liweze kujiendesha, hatutakubali kuliona linapata hasara baada ya uwekezaji mkubwa tulioufanya”