Saturday , 24th Apr , 2021

Bayern Munich watatwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga leo endapo kama watashinda mchezo wao wa leo dhidi ya Mainz, mchezo utakao chezwa majira ya Saa 16:30 Jioni, na huu utakuwa ni ubingwa wao wa 31 na wa 9 mfululizo wa Ligi Kuu.

Bayern Munich

Bayern wanaongozi ligi kwa tofauti ya alama 10 dhidi ya RB Leipzig walio nafasi ya pili na imesalia michezo minne kabla ya ligi kumalizika. Bayern wana alama 70 kwenye michezo 30 wakati RB leipzig wana alama 61 wakiwa na idadi sawa ya michezo.

Maiz watakuwa wenyeji wa The Bavarians katia dimba la Opel, na kama Bayern wakiibuka na ushindi katika mchezo huu watafikisha alama 74 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile kulingana na idadi ya michezo iliyosalia kabla ya ligi kumalizika.

Wapinzani wa karibu wa The Bavarians ,RB Leipizig hata wakishinda michezo yote iliyosalia watamaliza na alama 73 hivyo hawezi kufikia alama ambazo atakuwa nazo Bayern endapo kama wakishinda mchezo huu.

Huu utakuwa ubingwa wa tisa (9) mfululizo wa Ligi kuu Ujerumani ‘’Bundesliga’’ kwa Bayern Munich ambapo wameutetea ubingwa huu kwa misimu nane (8) mfululizo kuanzia msimu wa 2013-14.

Pia The Bavarians ndio mabingwa wa kihistoria wa Bundesilga wakiwa wametwaa mara 30, ikiwa ni mara nyingi kuliko timu yoyote ile nchini Ujerumani.