
Julian Nagelsmann
Nagelsmann mwenye umri wa miaka 33 amesaini mkataba wa miaka mitano na The Bavarians anachukua nafasi ya kocha Hansi Flick ambae ataondoka mwishoni mwa msimu.
Nagelsmann alifikia makubaliano binafsi ya kujiunga na mabingwa hao wa Ujerumani jana Jumatatu Aprili 26 kabla ya kuthibitishwa hii leo kuwa kocha mpya.
Inaripotiwa the Bavarians imelipa pauni million 21.7 ambayo ni zaidi ya bilioni 50 kwa pesa za kitanzania kama sehemu ya fidia ya kuvunja mkataba wa kocha huyo ambaye mkataba wake na RB Leipzig ulikuwa unamalizika mwaka 2023.
Taarifa hizi pia ni pigo kwa Tottenham HotSpurs ya England ambayo ilikuwa imeonyesha nia ya kumuwania kocha huyo.
Kwa sasa Spurs ipo chini ya kocha wa muda, Ryan Mason baada ya kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao mkuu Jose Mourinho, na sasa nguvu wanaamishia kwenye machuguo mengine wakiwa makocha kama Brendan Rodgers (Leicester City), Maurizio Sarri (Huru) na Rafa Benitez (Huru).
Julian Nagelsmann anatajwa kuwa kocha bora kijana kwa umri wake wa miaka 33,na mpaka hii leo ameiongoza RB Leipzig kwenye michezo 90 huku akishinda michezo 53 kati ya hiyo sare michezo 21 na amepoteza michezo 16, akiwa na wastani wa asalimi 58 ya ushindi katika kipindi cha miaka miwili.