
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zuberi.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mufti amesema kuwa baada ya kufanya ibada ya kuomba kuepushwa na madhara yatokanayo na majanga yoyote, Watanzania wanapaswa kufanya ibada ya shukrani pia.
"Watanzania tufanye ibada ya shukrani baada ya mwenyezi Mungu kuepusha madhara ambayo yangeweza kuikumba nchi kama Kimbunga Jobo kingejitokeza kama ilivyotarajiwa, tukijibiwa maombi tujifunze kushukuru", amesema Mufti.
Katika hatua nyingine amewataka Waislamu kutumia mwezi huu wa mtukufu kufanya ibada na kuliombea taifa kudumisha amani, umoja mshikamano na upendo.