Wednesday , 28th Apr , 2021

Timu ya Rhino Rangers ya Tabora imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya kombe la Shirikisho la Azam kwa kuwafunga Arusha FC 2-1.

Kikosi cha Arusha Fc kilichopoteza dhidi ya Rhino Rangers 2-1

Rhino Rangers wanakuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hii ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania,ambayo pia hutoa muwakilishi wa nchi katika mashindano ya Shirikisho la soka barani Africa 'CAF'

Hatua hii ya imezikutanisha timu mbili toka daraja la kwanza na hivyo kuonekana kufanana kwa viwango vyao, tofauti na baadhi ya mechi za mashindano haya zinapohusisha timu za madaraja tofauti kiwango huwa si bora

Kuelekea mechi hizi za mashindano ya kombe la shirikisho macho na masikio ya wadau wa soka, yapo katika mechi ya ijumaa kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga

Hii ni kutokana na aina ya mchezo wa nguvu wanaocheza Tanzania Prisons wanapokutana na timu hizi kubwa, huku Yanga ikihitaji kuchukua ubingwa huo ili angalau kuwa na uhakika wa kuwakilisha kimataifa , kwa kuwa upande wa ligi kuu upinzani ni mkubwa sana kutoka kwa mahasimu wao Simba