Thursday , 6th May , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Mei 7, 2021, anatarajiwa kufanya mkutano na zaidi ya Wazee 900 wa Mkoa wa Dar es salaam ambapo Katika kikao icho watajadili Mambo mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Akitoa taarifa ya Mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge, amesema kikao  hicho kitafanyika Ukumbi wa Mikutano Mlimani City kuanzia saa 8:00 Mchana.

Aidha RC Kunenge ametoa wito kwa Wazee waliopata mialiko ya kushiriki kikao hicho, kujitokeza kwa wingi ili wapate kusikiliza kile ambacho Rais Mhe. Samia amewaitia.

Kwa upande wao Viongozi wa Wazee wamemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuona umuhimu wa kukutana na Wazee huku wakisema wanatarajia Kikao icho kitakuwa na Manufaa makubwa kwao.