Thursday , 6th May , 2021

Kwenye mashindano ya riadha “Tokyo Olympics” washiriki hawataruhusiwa kuvaa mavazi yenye ujumbe wa "Black Lives Matter" wala kupiga magoti kwenye sherehe za michezo msimu huu wa joto.

Tokyo Olympics

Kamati ya Olympic (IOC) ilifafanua sera yake wiki mbili zilizopita kuwa hakutakuwa na maandamano kwenye uwanja wa michezo, wakati wa sherehe rasmi au kwenye jukwaa, lakini wiki hii maafisa wamethibitisha mavazi ya "BLM" yamejumuishwa katika marufuku hayo.

Hata hivyo maafisa, wamesema itikadi za "BLM" zitaruhusiwa sehemu zingine za michezo kama vile kwenye mikutano ya waandishi wa habari, wakati wa mahojiano na kwenye mikutano ya timu.