Friday , 18th Jun , 2021

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, ametoa wito kwa wadau wa elimu waliojitokeza katika mkutano wa kupokea maoni ya kuboresha mitaala nchini, kutoa maoni yatakayojikita kuwajengea wahitimu ujuzi na stadi zitakazoweshe kujitegemea.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Prof. Ndalichako amesema ni matarajio kuwa maoni yatakayopatikana kutoka kwa wadau mbalimbali yatasaidia kujibu changamoto ya wahitimu kumaliza kisha kusubiria matangazo ya kazi badala ya kujiajiri wenyewe.

"Wadau wamekuwa na wito kuwa na mitaala ya kuwaandaa vijana kujitegemea kujiajairi au kuajiriwa, ni imani yangu kuwa kupitia mkutano huu mtatoa maoni na mapendekezo yanayolenga kujibu changamoto hii pia suala hili tuliwekee mkazo kwa sababu ni kilo cha wadau kuwa wahitimu wanamaliza wanasubiri tu matangazo ya kazi," amesema Prof. Ndalichako.

Awali akizungumza Prof. Ndalichako amesema serikali imejikita katika kujenga uchumi wa viwanda hivyo kuna budi kuwa na wahitimu wabunifu watakosaidi kukuza uchumi wa nchi.

"Tumejikita katika kujenga uchumi wa viwanda, lazima tuzalishe wahitimu wabunifu wa waweze kubuni vyanzo zaidi vya kukuza na kuimarisha uchumi wa taifa, taifa lisilo na wahitimu mahiri kamwe haliwezi kusonga mbele," amesema Prof. Ndalichako.

Aidha, Prof. Ndalichako amaeto wito kwa taasisi za elimu ya juu nchini kuendesha mijadala ya kupitia mitaala kwani itawasaidia kukusanya maoni na kuyafanyia maboresho.

"Nitoe wito kwa taasisi za elimu ya juu nchini waanzishe mijadala kama hii, na kupata maoni kwa wadau mjielekeeze kushirikiana na taasisi binafsi muweze kujua mataraijio ya wahatimu ili nanyi kuingia kazini kutazama kwa kina," amesema Prof Ndalichako.

Leo Prof. Ndalichako alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu uboreshaji wa mitaala ya elimu ya awali, msingi na sekondari ulioandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania nchini (TET).