Thursday , 24th Jun , 2021

Uwepo wa lebo za muziki imara hapa nchini (licha ya kuwa ni chache) umesaidia kwa kiasi kikubwa kuibua na kukuza wasanii wapya ambao wanafanya poa sokoni kutokana na uwekezaji unaofanywa na kampuni hizo za kusimamia shughuli za muziki.

Picha kushoto Jay Melody, Wini (katikati) na Marioo (kulia)

Hali hiyo unaweza kusema kama imewapa hasira wasanii independent (wasio na lebo) ambao wapo wengi na wamelishika soko haswaa licha ya kuwa hawana backups zenye nguvu na uwezo wa kifedha.

Idadi kubwa ya wadau wa muziki wameonesha mabadiliko na ku-focus kwa wasanii wanaofanya kazi nzuri bila kujali kelele (kiki) au yupo katika hali gani na anatokea wapi.

Miongoni mwao ni;

1.Jay Melody
2.Marioo
3.Wini
4.Mabantu (kundi)