Haji Manara
Haji amesisitiza waamuzi wafate taratibu na sheria kwa kuzingatia sheria 17 za mpira wa miguu ili kutenda haki kwenye mchezo huo
“Wawa akicheza madhambi ya kupewa kadi nyekundu inayostahili kadi nyekundu ya moja kwa moja apewe hapo hapo, Onyango akifanya madhambi kwenye boksi la penati kamchezea mchezaji wa Yanga itolewe penati na kadi nyekundu, kadi hata nne, tatu nyekundu zitolewe lakini hivyo hivyo kwa wapinzani wetu yani nachokusudia kusema wasitake kuleta usawa, waamuzi wakachezeshe tu kwa mujibu wa sheria 17”. amesema Haji Manara
Kwenye michezo kadhaa iliyokutanisha timu hizi kongwe hapa nchini kumekuwa na malalamiko kwa waamuzi kwenye kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu, na kushuhudia matukio tata kwenye michezo hiyo. N a katika michezo mitaatu ya Ligi Kuu ya mwisho timu hizi kukutana zimetolewa penati mbili ambazo zote zilikuwa na malalamiko, moja ilikwenda kwa Simba na moja kwa Yanga.
Timu hizi zinaingia kwenye mchezo huu zikiwa zinatofautiana alama sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu, Simba wakiwa vinara kwa alama 73 wakati Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 67, na endapo kama Simba wakishinda mchezo huu watafikisha alama 76 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile hivyo watatangazwa kuwa mabingwa wa VPL kwa msimu wan ne mfululizo.
Mchezo huu uachezwa uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam na utaanza kutimua vumbi majira ya Saa 11:00 Jioni. Na utaskiliza matangazo ya mchezo huu moja kwa moja kupitia East Africa Radio.




