Friday , 2nd Jul , 2021

Kupitia kipindi maalum cha siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan kilichoruka Alhamisi Julai 1, 2021 saa 3:00 usiku ndani ya East Africa Television, Mwanadiplomasia Severin Kapinga, ameeleza faida za ziara za Rais Samia.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu (kushoto) na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kulia)

Kapinga amesema kuna faida kadhaa ambazo zimepatikana kwa taifa kutokana na ziara mbalimbali za Rais Samia ndani ya muda wa siku 100 za uongozi wake haswa mahusiano mazuri na mataifa jirani kama Kenya, Uganda na Rwanda.

Ameongeza kuwa katika kuboresha uchumi wa viwanda ni lazima kutengeneza ushirikiano na washindani ndio maana ziara yake nchini Kenya ilikuja na majibu ya kizuizi cha bidhaa kwenye mipaka ya nchi hizo mbili na hatimaye wafanyabiashara wa Tanzania wakaanza kuingiza mahindi Kenya.

Zaidi tazama video hapo chini akieleza.