Monday , 5th Jul , 2021

Kutoka mitandaoni kuna 'video clip' ili-trend ikimuonesha Michael Jackson akimsifia mama yake mzazi kwenye harusi kuliko mkewe ambapo baadhi ya watu wamejaji tukio hilo kwa kusema sifa hizo alizotoa ilibidi ziende kwa mke wake.

Picha ya Michael Jackson na mke wake

Akijibu suala hilo kupitia EATV & EA Radio Digital kwa njia ya mtandao wa WhatsApp Michael Jackson amesema 

"Jamii inaishi kwa mitazamo waitakayo, mazoea na kukariri baadhi ya vitu, ukitaka kuwaridhisha hutoweza na utakua mtumwa katika kuishi maisha yako na kile unachokiamini, nafasi ya wazazi inabaki kwenye nafasi yao na mke ana nafasi yake"

"Kumsifia mke hakuondoi upendo,shukran na thamani ya wazazi na kuwasifia wazazi hakuondoi thamani na upendo kwa mke, lazima watu waelewe hakuna muda maalumu au siku maalumu anayostahili kupongezwa mzazi, mke au mume, sema mazuri ya mtu popote unapopata nafasi akiwa anasikia kwani hakuna aijue kesho" ameongeza 

Pia ameendelea kusema yeye na mke wake wanajuana vizuri na hawaishi kwa matarajio ya watu bali wanaishi kwa uhalisia ya maisha yao.